April 26, 2013



Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema Yanga walistahili kuwa mabingwa wa Tanzania Bara.

Hall raia wa Uingereza amesema Yanga walibadili gia na kupata pointi nyingi mapema lakini akakipongeza kikosi chake cha Azam FC kwa kuwa washindani pekee wa Yanga kwa kipindi kirefu.


“Mwenzako akishinda unapaswa kumpongeza, huo ndiyo uanamichezo. Walijipanga mapema hasa baada ya kuanza msimu vibaya.

“Lakini Azam ilifanya vizuri pia na ndiyo imekuwa mshindani mkubwa wa Yanga kwa kipindi kirefu. Zaidi walituhofia sisi hadi siku ya mwisho.

“Wachezaji wangu walijitahidi kadri ya uwezo wao, nawapongeza ingawa tungeweza kufanya vizuri zaidi ya hapo,” alisema Hall.

Azam FC imeendelea kubaki kwenye nafasi yake ya pili ambayo iliishika msimu uliopita na Yanga ikashuka hadi namba tatu ikishika nafasi hiyo tokea mwaka 1988.

Safari hii, Yanga imekuwa bingwa, Azam FC imebaki katika nafasi ya pili huku ikionekana Simba inahitajika kufanya kazi ya ziada kushika nafasi ya tatu, la sivyo Kagera Sugar, Mtibwa Sugar au Coastal Union wataichukua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic