Sare ya mabao 1-1 kati ya Coastal Union na Azam FC imeipa Yanga ubingwa
wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga imekuwa bingwa kwa kufikisha pointi 56 ambazo tayari ilikuwa nazo
na Azam FC ndiyo ilionekana kuiopa presha.
Lakini sare hiyo ya leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga
imeiruhusu Yanga kubeba taji hilo kwa kuwa Azam haiwezi kufikia.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ameiambia Salehjembe kuwa ubingwa huo
mapema wakiwa na mechi mbili mkononi ni matokeo ya kazi na umoja.
“Mkishirikiana siku ya mwisho mnapata matunda bora, ushindi umekuja
tukiwa hatuchezi na tumepumzika.
“Hayo ni matokeo ya kujituma lakini bado nitafurahi tukishinda mechi
mbili zilizobaki dhidi ya Coastal Union na Simba,” alisema Brandts raia wa
Uholanzi.
Katika mechi hiyo ya Mkwakwani, Azam walitangulia kufungwa kwa mkwaju wa
penalty kupitia kwa beki wake Agrey Morris lakini Coastal wakasawazisha kupitia
Daniel Lyanga aliyekuwa ameingia kipi cha pili.








0 COMMENTS:
Post a Comment