Mke wa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig ametua jijini Dar es Salaam
na kuungana na mumewe.
Mke huyo yuko nchini kwa zaidi ya wiki tatu akiishi na mumewe ambaye
anaendelea kazi ya kuinoa Simba.
Pamoja na kukubali mkewe yuko Dar pamoja naye, lakini Liewig raia wa
Ufaransa hakutaka kuzungumzia zaidi.
“Kweli yuko hapa, siku chache zijazo ataondoka lakini vizuri
tukazungumzia mambo mengine,” alisema.
Hata hivyo, mambo yamekuwa hayaendi vizuri katika kikosi hicho cha
Msimbazi kinachotumia vijana wengi zaidi.
Liewig ambaye alichukua nafasi ya Milovan, tayari amekubali kuwa kikosi
chake hakina nafasi ya kuchukua hata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu.
Yanga wameishatangazwa kuwa mabingwa, Azam FC imejihakikishia nafasi ya
pili na Simba inaendelea kuwania nafasi ya tatu ikichuana na Kagera Sugar na
Coastal Union.







0 COMMENTS:
Post a Comment