Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen
ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia
wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim
amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza
wachezaji.
Amesema timu hiyo inajumuisha
wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya
kuingia Taifa Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.
“Timu hii ni kiungo kati ya vijana
na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache
watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi
kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa
Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.
Young Taifa Stars yenye wachezaji 30
itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka
huu.
Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula
(Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa.
Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza),
Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam
(Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam)
na Emily Mgeta (Simba).
Viungo ni Haruna Chanongo (Simba),
Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba),
Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu),
Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent
Barnabas (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni Hussein Javu
(Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha
Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).







0 COMMENTS:
Post a Comment