Si kitu cha ajabu kwa kuwa katika mechi nyingi za Ligi Kuu Bara, mambo yanakuwa kama unavyoona.
Listi ya wachezaji wa timu zote mbili huandikwa kama unavyoona, kitu ambacho si sahihi.
Karatasi hii ni ya majina ya wachezaji wa Mgambo Shooting na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 1-1, listi iliandikwa kwa mkono kama unavyoona na ndiyo mambo yamekuwa yakiendelea mikoani katika mechi karibu zote.
Karatasi hii inaweza ikawa inaonyesha namna gani mambo mengi katika ligi hiyo na hasa katika mechi za mikoani yamekuwa yakifanya kwa kubabaisha.
Listi za Dar es Salaam, zinaandikwa kwa mpangilio mzuri. Mambo mengi ya Dar yanakwenda kwa mpangilio mzuri.
Iko haja ya kulifanyia kazi suala hilo ili kuonyesha ligi hiyo inajumuisha watu makini na wanaoijua kazi yao.








0 COMMENTS:
Post a Comment