| van Persie |
Mwandishi Wetu
NAJUA makala hii inaweza kuzusha ubishi mkubwa hapo ulipo kama utakuwa
na wenzako ambao ni wadau wa soka pia, wapo wanaodai kuwa kufunga bao kwa
penalti ni bahati, lakini wengine wanaamini uwezo wa kupiga penalti nao
unachangia.
Kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kupiga penalti duniani, wafuatao
wanatajwa na wengi kuwa uwezo wao ni mkubwa zaidi ya wengine;
Robin Van Persie
Staa wa Man United ana uwezo mkubwa kwa kutumia mguu wa kushoto kupiga
penalti, yeye na Wayne Rooney ndiyo wenye jukumu hilo klabuni hapo.
Graham Alexander
Beki wa pembeni ambaye hakuwa na jina kubwa, baadhi ya timu alizopita
ni Burnley na Preston North End zote za England.
Mario Balotelli
Anaonekana kama ‘chizi’ lakini akisimama mbele ya 18 anajua wapi pa
kupiga, kwa sasa anaichezea AC Milan.
Leighton Baines
Beki wa kushoto wa Everton ambaye pindi anapopiga penalti kwa mguu
wake wa kushoto ni vigumu kukosa.
Johan Cruyff
Alikuwa kocha mwenye mbinu nyingi lakini enzi zake za uchezaji pia
alikuwa mbunifu wa penalti. Jina lake litaendelea kukumbukwa daima kutokana na
mchango wake katika soka.
Gerd Muller
Ataendelea kukumbukwa siku zote nchini Ujerumani kutokana na uwezo
wake wa kufunga, Muller aliweza kufunga penalti nyingi katika maisha yake ya
soka.
Ronaldinho
Enzi zake alikuwa mwepesi na mjanjamjanja awapo na mpira.
Gary McAllister
Alicheza klabu nyingi lakini akiwa Liverpool alipata heshima kwa kuwa
alikuwa na uzoefu zaidi. Aliwahi kukosa penalti muhimu katika michuano ya Ulaya
1996 alipokuwa akiichezea Scotland dhidi ya England.
Eric Cantona
Aliyekuwa kijana mtukutu lakini mbele ya lango hakuwa na utani kabisa,
alifunga penalti nyingi pia.
Andrea Pirlo
Mashabiki walioshuhudia michuano ya Euro 2012 wanajua ‘muziki’ wake,
alipiga penalti akiwa kwenye kikosi cha Italia kilipocheza dhidi ya England,
ambapo alikuwa kama anapiga shuti kisha akapiga taratibu huku akimuacha kipa
Joe Hart ‘akipotea vibaya’.
Michael Ballack
Kiungo wa Ujerumani ambaye alikuwa akicheza soka la nguvu, alikuwa na
uwezo mzuri wa kupiga penalti, jukumu alilofanya akiwa klabuni na timu ya taifa.
Michel Platini
Rais wa sasa wa Uefa ambaye alisaidia Ufaransa kutwaa ubingwa wa Euro 1984,
alikuwa na mbinu kali kila alipokwenda kupiga penalti.
Steven Gerrard
Nahodha mkongwe wa Liverpool ambaye wapo wanaomuita kwa jina la utani
la Mr Liverpool, ana uzoefu wa kupiga penalti na amekuwa akipiga vizuri licha
ya kuwa amewahi kukosa mara kadhaa.
Alessandro Del Piero
Aliifungua Juventus na timu ya taifa ya Italia mara nyingi.
Cristiano Ronaldo
Amefunga mabao mengi kwa njia ya penalti, siyo mtaalam sana ila ni
nadra kukosa, amefanya vizuri akiwa Man United, Real Madrid na timu ya taifa ya
Ureno.
Frank Lampard
Kiungo mkongwe wa Chelsea ambaye jukumu la kupiga penalti anapewa
yeye.
Zinedine Zidane
Kitendo cha kumpiga kichwa Marco Materazzi mwaka 2010 kinakumbukwa
zaidi, lakini wanaomfuatilia wanajua alivyokuwa bora kwenye penalti.
Alan Shearer
Nguli wa Newcastle ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa penalti.
Matthew Le Tissier
Hajulikani kwa kiwango cha juu, aliwahi kukosa penalti moja tu kati ya
43 alizopiga katika maisha yake ya soka la kulipwa. Tissier, 44, aliichezea
Southampton kuanzia mwaka 1985 mpaka 2002 na kufunga mabao zaidi ya 161. Bahati
mbaya ni kuwa aliichezea timu ya taifa mechi nane tu.













0 COMMENTS:
Post a Comment