Liverpool imeendelea kuonekana ina bahati mbaya baada ya kumkosa beki wa kati wa Vasco, Dede ambaye ameamua kubaki Brazil na kujiunga na Cruzeiro.
Dede ndiye alikuwa chaguo la kwanza la Kocha, Brendan Rogers katika uhamisho wa majira ya joto.
Rogers alikuwa amemlenga Dede kwa kuwa safu yake ya ulinzi imeonekana kutokuwa na mhimili na hivi karibuni mkongwe, Jamie Carragher atajiuzulu.
Wakala wa Dede, Giuliano Aranda amesema mchezaji huyo kisiki wa kimataifa wa Bazil alikuwa na uwezo wa kuchagua na mwisho ameamua kubaki Brazil.
Maana yake Liverpool italazimika kuanza kusaka upya beki atakayechukua nafasi huyo kwa kuwa lazima itasajili beki wa kati.
Cruzeiro imetoa pauni milioni 4.2 kumpata beki huyo ambaye awali aliwahi kuwania na magwiji wa soka la Ulaya kama Manchester United na AC Milan.







0 COMMENTS:
Post a Comment