FULL TIME
Dk 5 za nyongeza.
Dk 87, Dihile anaokoa shuti kali la Nizar na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda
Dk 5 za nyongeza.
Dk 87, Dihile anaokoa shuti kali la Nizar na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda
Dk 80, Ruvu wamepotea, Dihile anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali
la Nizar
Dk 73, Dihile anafanya kazi ya ziada kumzuia Msuva baada ya kupokea pasi
ya Niyonzima.
Dk 68-71 Yanga wanafanya mashambulizi mfululizo lakini wanakosea katika
kumalizia.
GOOOOOOO..Dk 64 Nizar anaifungia Yanga bao la tatu baada ya kufanya
shambulizi kali na Domayo kupiga mpira uliogonga mwamba na kumkuta mfungaji.
GOOOOOOOO..Dk 58 Kiiza anaifungia Yanga bao la kichwa baada ya krosi
safi ya mpira wa faulo ya David Luhende
Dk 52, Kiiza katika nafasi nzuri huku mabeki wa Ruvu wakidhani ameotea,
anapiga shuti kuuuuubwaaaaa juu.
Dk 50, Cannavaro anaokoa shuti la Mgisa na kuwa kona ambayo barthez
anaihifadhi.
Dk 46, nizar anawatoka mabeki watatu na kupita shuti linalotoka
sentimeta chache pembeni
HALF TIME:
Baada ya filimbi ya mapumziko, wachezaji wa Ruvu wanaanza kuzozana
katikati ya uwanja kabla ya kuingia vyumbani.
GOOOOOOOOOOO Dk 45, Msuva anaifungia Yanga bao baada ya kuuwahi mpira wa
kurusha huku mabeki wa Ruvu wakidhani ameotea na mwamuzi Oden Mbaga anasema, “weka
kati”.
Dk 42, Ruvu wanaonekana kupoteza muda kama wanahitaji sare
DK 37, Pazi anapoteza nafasi nyingine kwa kushindwa kuupiga mpira
Dk 35, lango wazi la JKT, Kiiza anapiga shuti nje.
Dk 32, Mgosi anapiga shuti kali baada ya kumtoka Yondani, lakini
halikulenga goli.
Dk 31 Msuva anapiga shuti kali linalogonga mwamba na kurudi uwanjani.
Dk 30, Nizar anawapiga chenga mabeki wa Ruvu na kuachia shuti la chini,
Dihile anatoa na kuwa kona.
Dk 25, Pazi anapiga shuti safi baada ya kumhadaa Twite lakini linatoka
nje
Dk 24, Mgosi anawahadaa mabeki wa Yanga na kupiga shuti hafifu
linalodakwa kilahisi
Dk 22, mpira wa faulo wa Luhende unatua kichwani mwa cannavaro, unatoka
sentimeta chache.
Dk 21, krosi ya Twite, kipa dihile anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira
kichwani mwa kiiza.
Dk 19 Chuji anapoiga shuti kali linatoka sentimeta chache.
Dk 16, pasi nzuri ya Nizar, mita tatu kutoka langoni Kiiza anapiga shuti
lakini beki Makwaya analala na kuokoa, inakua kona tasa.
Dk 12 Makwaya anapiga shuti hafifu baada ya pasi nzuri Mgosi, kipa
Barthez analidaka kwa ulaiiniii.
Dk 9, Nizar anageuka na kupiga vizuri baada ya kuwahadaa mabeki wa Ruvu
lakini anashindwa kulenga lango
Dk 7, shuti kali ya Twite linapita juu ya lango ilikuwa ni baada ya pasi
nzuri ya Msuva.
Dk 5, Dihile anaikuka na mechi inaendelea
DK 1-3, Yanga wanapata kona tatu ambazo zote zinakuwa tasa ni baada ya
kufanya mashambulizi mfululizo. Kipa wa JKT, Dihile yuko chini baada ya
kugongana na Nizar.
Mpira umeanzam Yanga inapeleka mashambulizi kaskazini na Ruvu kusini.
RUVU JKT:
Dihile, kikutwa, nkomola, madenge, makwaya, naftary, mgisa, mkanga,
mgosi, pazi na adolf (C)
YANGA:
Barthez, twite, luhende, cannavaro (C), yondani, chuji, msuva, domayo,
kiiza, nizar na niyonzima







0 COMMENTS:
Post a Comment