Mechi
tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe
moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini
sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.
TFF ilibadilisha ratiba na kuingia kwenye mgogoro mkubwa na klabu kutokana na kubadili ratiba ili kuipa nafasi SuperSport kuonyesha lakini ndiyo imetoa nje.
Kwa
mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya
Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo
kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB
van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.
Mechi
hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba,
Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17
mwaka huu jijini Tanga.
Tatizo
hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana
wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi
hiyo ya Kenya.
Tshunungwa
amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo.
SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine
za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.
Pia
TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa
habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment