LIVERPOOL YAIKOMALIA CHELSEA MWISHONI Mshambuliaji Luis Suarez amefunga bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza na kuinyima Chelsea raha ya ushindi. Chelsea walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1 hadi dakika ya 90 zilipoongezwa dakika sita. Bao la hilo la kichwa, liliondoa raha ya ushindi na Liverpool wakawa wanashangilia sare hiyo. Bao la kwanza la Liverpool lilifungwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Sturridge. Mabao mawili ya Chelsea yalifungwa na Oscar na Hazard kwa mkwaju wa penalti.
0 COMMENTS:
Post a Comment