SUAREZ ATOA KALI YA MWAKA, AMUUMA BEKI WA CHELSEA Hii kali ya mwaka, mshambuliaji wa Liverpool alitia kali ya mwaka baada kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic. Suarez ambaye ni mbaguzi mkubwa wa rangi na mtukutu, alimuuma Ivanovic wakati wanawania mpira. Hata hivyo, mwamuzi wa mchezo huo hakuweza kuona vizuri na mwisho Ivanovic akaishia kulaumu. Lakini picha mnato na zile za video zilimuonyesha Suarez akimg’ata Ivanovic hali iliyowashangaza wengi. Baadhi ya mitandao ya kijamii wameanzisha utani kwamba hata muonekano wa meno ya mshambuliaji huyo yamekaa ki “kuuma uma” tu!.
0 COMMENTS:
Post a Comment