April 21, 2013



Kipigo cha mabao 3-1 ilichokitoa Tottenham Hotspur kwa Man City, maana yake ubingwa uko mikononi mwa Man United .

United iko kileleni na pointi 81, wakati Man City ina pointi 68, maana yake kama United ikishinda na kufikisha pointi 84 itakuwa imejihakikishia kuwa bingwa.





Maana City ikishinda mechi zake tano zilizobaki itakuwa na pointi 83, maana yake ushindi wa mechi moja tu kati ya tano ilizobakiza United ni kitu kinachowezekana.


Katika mechi ya leo, Spurs iliyokuwa nyumbani ilionekana kwua moto wa kuotea mbali.


 

Dempsey, Defoe na Bale ndiyo walikuwa wabaya wa City baada ya kupachika mabao hayo.

City walitangulia kwa bao la Nasri lakini baadaye walionekana kuishiwa upepo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic