Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga leo walifanya mazoezi mepesi
katika Gym mpya ya kisasa katika eneo la Quality Centre jijini Dar es Salaam.
Yanga walifanya mazoezi katika gym hiyo mpya ya kisasa inayojulikana kwa
jina la Rio.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts alisema hiyo ni sehemu ya programu ya
kikosi chake.
“Baada ya gym, Jumatatu na Jumanne tufanya mazoezi ya uwanjani kama
kawaida kujiandaa na mechi ya Jumatano.
“Gym ina vifaa vya kutosha na imenivutia sana, nilitamani ingekuwepo
tokea mwanzo,” alisema.
“Wakati wa kujiandaa na msimu mpya tutaitumia zaidi kwa kuwa kuna kila
kitu kinachotakiwa kwa ajili ya mazoezi,” alisema Brandts raia wa Uholanzi.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA MENEJA WA YANGA, HAFIDHI SALEH













0 COMMENTS:
Post a Comment