Ukihesabu utaona
wachezaji waliopo ni 26, pamoja na viongozi wanne walio katika picha hii.
Ukitaka kujua
timu zetu za Tanzania zinabahatisha mambo mengi, ngoja nikupe ufafanuzi wa hili
linalofuata.
Ndani ya
miaka minne tu, kati ya wachezaji hao 26 walio katika kikosi cha Simba msimu
huu ni wachezaji sita tu. Maana yake 20 wote walishaondoka ndani ya miaka hiyo.
Hao sita
waliobaki ni Juma Kaseja, Ramadhani Shamte, Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’,
Amri Kiemba na Ramadhani Chombo ‘Redondo’.
Katika hao
sita waliobaki, wenye uhakika wa kucheza katika kikosi kilicho chini ya
Mfaransa ni wawili tu, Kaseja na Kiemba. Upande wa Shamte, yeye ni mtu
anayetafuta namba.
Wengine watatu,
yaani Nyosso, Redondo na Boban wao wamesimamishwa kwa madai ya utovu wa nidhamu
sasa takribani mwezi.
Lakini
hadi leo uongozi na benchi la ufundi wamekuwa wakitupiana mpira kila upande. Maana
uongozi unasema utaliambia benchi la ufundi litoe maelezo lakini hadi sasa
haujatoa.
Si kitu
lahisi, benchi la ufundi likamsimamisha mchezaji lakini lisitoe maelezo kwa
uongozi kwa zaidi ya mwezi na mshahara mchezaji anaendelea kuchukua.
Hali hii
inaonyesha kuna mambo mengi sana ya kubabaisha, huenda uongozi ni tatizo lakini
pia wachezaji wanaweza wakawa wanaguswa.
Ndani ya
misimu mitano, wachezaji 26 waliopo ni sita tu na kati yao hao, wanaocheza ni
wawili tu na wengine hawana nafasi.
Unaweza kusema
wachezaji 24 hawana nafasi na wawili tu ndiyo wanaocheza.
Kwa upande
wa viongozi wanne, wawili bado wanaendelea kubaki Simba ambao ni daktari Cosmas
Kapinga na Amri Said ambaye yuko katika timu ya vijana.
Aliyekuwa
Meneja, Innocent Njovu hayupo kama ilivyokuwa kwa Kocha Mkuu wakati huo,
Patrick Phiri.
Kuna mambo
mengi ya kuangalia, wachezaji lazima wadumishe viwango vyao lakini inaonekana
suala la propaganda ya usajili linaziathiri timu.
Iko namna
hii, kila unapofika wakati wa usajili, timu hutaka kuonekana magazetini na
kwenye vyombo vya habari imefanya usajili wa kutisha.
Hivyo wanasajili
hovyo, wanaacha wachezaji hovyo na hakuna uvumilivu hata kidogo.
Kama kuna
mchezaji alifanya kosa moja katika mchezo fulani wa ligi, bila ya kuamini soka
lazima liendane na makosa, basi anaondolewa mara moja na timu inafanya usajili wa
kumchukua mchezaji ambaye huenda kiwango kinaendana tu au aliyesajiliwa anakuwa
na kiwango cha chini zaidi.
TAFAKARI…NDIIIIIIII!








0 COMMENTS:
Post a Comment