Ilionekana
ni kama kitu cha ajabu, lakini ndiyo hali halisi, si hadithi. Bayern Munich
imeifunga Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona
pamoja na kuwa na Lionel Messi imejikuta inaogelea kipigo hicho cha aibu mjini
Munich kwa kuchapwa mabao hayo.
Wajerumani
hao wangeweza kushinda hata mabao saba, lakini mpira ndivyo ulivyo.
Mabao ya
Bayern iliyokuwa nyumbani yalifungwa na Muller aliyefunga la kwanza na la nne
katika dakika ya 25 na 82.
Gomez
alifunga la pili katika dakika ya 49 na mkali, Robben yeye alifunga la tatu.
Angalia picha
za action namba Barca walivyokuwa wanapelekwa puta kama watoto wa ‘shule’.
















0 COMMENTS:
Post a Comment