Uongozi wa Yanga umetaka kupewa muda zaidi ili kuchagua ramani ya uwanja
inaoutaka.
Awali uongozi wa Yanga ulitangaza kuwa siku saba tu zilikuwa zinatosha
kabla haijachagua inataka ramani ipi kati ya tatu ilizopewa na kampuni ya
Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China.
Akizungumza kutoka China, Meneja wa BCEGC aliyejitambulisha kwa jina
moja la David alisema mambo yanakwenda vizuri na wameamua kuwapa Yanga muda
zaidi.
“Ni jambo la msingi wawe na muda zaidi ya kuchagua kutokana na uwezo
wao, eneo lao na mambo mengi ya kitaalamu yanatakiwa.
“Tunajua wanalazimika kukutana na kujadili, wiki moja isingetosha,
lakini hata wao wameona hivyo. Maana yake tunaenda vizuri,” alisema David
ambaye alisema anarejea nchini baada ya siku chache.
BCEG iliyojenga Uwanja wa Taifa Dar, ilitoa ramani tatu kwa uongozi wa
Yanga na kuwapa muda wachague moja kati ya hizo.
Katika ramani hizo za uwanja utakaojengwa kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar, uwanja mkubwa una uwezo wa kuingiza watu 50,000
unafuatia unaobeba watu 40,000 na mwisho ni ule unaochukua watu 30,000.







0 COMMENTS:
Post a Comment