Hatimaye
sasa kila kitu hadharani baada ya kubainika walibuaji wa mabomu katika mbio za
Boston Marathon ni ndugu raia wa Chechnya.
Tayari watu
wausalama wa Marekani wameanza mapambano nao na kufanikiwa kumuua mmoja aitwaye
Tamerlan
Tsarnaev, 26, ambaye ni mkubwa lakini katika mapambano hayo askari polisi mmoja
aliuwawa.
Mdogo wake
Dzhokhar Tsarnaev, 19, ambaye amekuwa
mtuhumiwa namba mbili bado anaendelea kutafutwa.
Kila kitu katika mji huo kimesimama kwa kuwa hakuna usafiri wa jamii kama
mabasi na treni.
Raia wameambiwa wasimfungulie mtu wasiyemjua na ndege zimetakiwa
kusitisha safari zake mara moja.
Taarifa za awali zinaeleza wawili hao wamekuwa wakiishi nchini Marekani
tokea mwaka 2002 na miaka 11 baadaye ndiyo wametimiza walichokuwa wanataka
kukifanya.
Tayari picha zao ziko mitaani na wananchi wameambiwa waendelee kutoa
msaada wa kuhakikisha anapatikana wakati akiendelea kusakwa kila moja.










0 COMMENTS:
Post a Comment