Makocha wawili wa Simba, bosi Patrick Liewig na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wamenuniana.
Liewig raia wa Ufaransa amekuwa haelewani na Julio ndani ya siku nne zilizopita lakini wao wamekuwa wakificha.
Hii si mara ya kwanza kwa Julio na Mfaransa huyo kununiana ingaw wao wamekuwa wakitaka kulifanya jambo hilo siri.
Katika mazoezi ya Simba, majukumu yote ambayo Liewig alikuwa akimpa Julio, sasa amegeuza njia na kuanza kuyakabishi kwa kocha wa makipa, James Kisaka.
Imeelezwa chanzo cha Julio na mzungu huyo kununiana ni baada ya msaidizi huyo kuchoshwa na kauli za ukali.
“Julio alifokea na mzungu, sasa akaona kama amchoka naye akajibu mapigo hivyo wakajibizana sana.
“Baada ya hapo tunaona wanasalimiana tu na baada ya hapo kila mtu anachukua time yake.
“Wakati fulani Julio ndiye alikuwa anampeleka kocha mazoezini lakini sasa hivi mambo yako tofauti kabisa. Kocha anapanda Hiace ya timu na Julio anachukua zake time.
“Lakini wakiulizwa kuhusiana na hilo wamekuwa hawataki kusema,” kilifafanua chanzo.
Taarifa nyingine za uhakika zimeeleza kesho kutakuwa na kikao maalum cha uongozi na Julio na Liewig watakutanishwa na suala hilo litajadiliwa ili kupata mwafaka.
Awali kulikuwahi kuwa na hali ya kutoelewana kati ya Julio na Meneja wa timu hiyo, Moses Basena raia wa Uganda lakini wamekuwa wakificha suala hilo na linaporipotiwa wanakuwa wakali sana.







0 COMMENTS:
Post a Comment