Kiungo wa Simba, Kiggi Makasi bado hana uhakika wa kupata matibabu ya upasuaji wa goti yaliyopangwa kufanyika nchini India.
Mwezi ulipoita, daktari mmoja maarufu alishauri Kiggi akafanyie upasuaji nchini India.
Lakini bado uongozi wa Simba chini ya Ismail Aden Rage umekuwa ukisuasua kuhusiana na suala.
Ingawa uongozi huo umekataa katakata kulizungumzia suala hilo, lakini inaonekana Kiggi yuko wakati mgumu.
“Kweli jamaa (Kiggi) anaumwa sana, lakini hakuna ambacho kinaeleweka wala mambo yaliyokaa vizuri.
“Amekuwa ni mtu mwenye hofu sana kwa kuwa hajui mwisho wake hasa utakuwa ni upi. Lakini tunajaribu kumpoza kama mdogo wetu,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Kiggi aliumia vibaya wakati Simba ikiwa njiani kwenda mjini Bukoba kuivaa Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Aliumia wakia mjini Dodoma wakati Simba ikicheza mechi za kuchangisha fedha ili iweze kujihudumia vizuri. Baada ya hapo akarejeshwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu na ushauri ukatolewa na daktari bingwa kwamba angepelekwa India kwa ajili ya upasuaji.







0 COMMENTS:
Post a Comment