![]() |
| Bale |
Wachezaji
wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu England (PFA) wametajwa.
Wachezaji
sita wametangazwa kuwania tuzo hiyo akiwemo kiungo wa Man United, Michael
Carrick ambaye hakutarajiwa.
Wengine
ni anayeshikilia tuzo hiyo, Robin van Persie, wengine ni Luis Suarez wa
Liverpool, mshambuliaji nyota wa Spurs, Gareth Bale na viungo wawili wa Chelsea,
Eden Hazard na Juan Mata.
Hakuna
beki wala kipa katika tuzo hiyo ambayo washindi hupatikana kwa wachezaji kupiga
kura tofauti na ile nyingine ambaye mshindi hupatikana kutokana na wadhamini,
msimu uliopita alishinda Vincent Kompany.
Blogu ya
Salehjembe imeamua kuchagua tatu bora yake na nafasi ya kwanza inakwenda kwa
Bale, Suarez halafu van Persie huku wachezaji wawili wa Chelsea wakishika
nafasi mbili za mwisho.










0 COMMENTS:
Post a Comment