April 2, 2013



 
Penzi la Mario Balotelli na mwanamitindo Fanny Neguesha limezidi kupamba moto baada ya wawili hao kuweka picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram wakila raha.

Kilichovutia zaidi ni kwamba, Fanny ambaye alikuwa amemkalia Balotelli alikuwa amevaa nguo yenye madoa ya kijeshi.


Kawaida Balotelli amekuwa akihakikisha vitu anavyovipenda vina rangi ya kijeshi kama alivyofanya katika gari lake la kifahari aina ya Bentley.


Penzi la Fanny na Balotelli limeshika kasi ikiwa ni siku chache baada ya mshambuliaji huyo wa AC Milan, kupigana kibuti na mzazi mwenzake Raffaella Fico ambaye amejifungua mtoto aliyepewa jina la Pia.
 
Raffaela
Fanny..
Hivi karibuni, Balotelli na Fanny walitokea katika ukurasa wa mbele wa jarida maarufu la watu maarufu la Vanity Fair na yeye alieleza namna penzi lao lilivyokolea.

Balotelli alisema anaamini huenda akamaliza maisha yake yote na Fanny ambaye amekuwa kipenzi chake.

Balotelli alikuwa gumzo wakati akiwa Man City lakini ameamua kureja Italia na safari hii amejiunga na AC Milan ambao ni wapinzani wakubwa wa timu iliyomkuza kisoka ya Inter Milan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic