April 7, 2019


KOCHA wa Singida United Fred Minziro amezidi  kupeta ndani ya kikosi hicho baada ya kupata ushindi wake wa pili mfululizo na kupandisha kikosi chake kutoka nafasi ya 15 mpaka ya 11.

Minziro alianza kushinda mbele ya Alliance kwa ushindi wa mabao 2-0 na jana aliibuka na ushindi mbele ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1.

Mabao ya Singida United yalifungwa na Kenny Ally, Himid Suleiman na lile la Kagera Sugar likifungwa na Omary Mponda 11 na kufanya mabo yazidi kuwa magumu kwa Kagera kwani mchezo wao uliopita mbele ya Azam FC walipoteza. 

Inashuka kutoka nafasi ya 13 mpaka nafasi ya 15 kwa sasa wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 31.

Lipuli FC ya Matola ilibanwa mbavu na Mwadui FC na ilikubali sare ya kufungana mabao 2-2, mabao ya Lipuli yalifungwa na Paul Nonga dk ya 60 na Issa Rashid dk 85 kwa upande wa Mwadui wafungaji walikuwa ni Wallace Kiango, Ditram Nchimbi 70.

 Mtibwa Sugar waliibana Alliance ya Mwanza kwa kuifunga bao 1-0 mpachikaji wa bao akiwa ni Jaffary Kibaya dk18.


Mohamed Abdallah alianza kwa ushindi na kuiongoza timu yake ya JKT Tanzania kuifunga bao 1-0 Mbeya City.

TZ Prisons 0-0 Biashara United na ziliweka rekodi ya kuingiza kiasi cha shilingi elfu tisa tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic