September 2, 2021

 


HERITIER Makambo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa malengo makubwa kwa msimu wa 2021/22 ni kuweza kusepa na mataji ambayo watashiriki ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara.

Makambo amerejea ndani ya Yanga aliyokuwa akiitumikia msimu wa 2018/19 kabla ya kuibukia ndani ya Horoya ya Guinea.

Waliweza kufikia makubaliano ya kuachana pande zote mbili kwa kuwa dili lake lilikuwa limebakiza mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo.

Baada ya kureja ndani ya Yanga inaelezwa kuwa ni dili la miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia. 

Makambo amesema:"Tupo imara na kwa namna ambavyo timu ipo tuna uhakika tutafanya vizuri, tunahitaji kuchukua makombe kwenye mashindano ambayo tutashiriki.

"Ipo wazi kwamba haitakuwa rahisi lakini ni lazima tujitume zaidi na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kufikia malengo ambayo tumejiwekea," .

Wakati anasepa nyota huyo alikuwa ni namba moja kwa utupiaji ambapo alitupia mabao 17.Anareja na kukuta namba moja kwa utupiaji kwa msimu wa 2020/21 ni Yacouba Songne ambaye alitupia mabao 8.

Mabingwa wa msimu uliopita wa 2020/21 ni Simba ambao pia walitwaa taji hilo zama zile wakati akisepa na timu ilimaliza ikiwa nafasi ya pili kama ambavyo ilifanya hivyo pia msimu uliopita.

4 COMMENTS:

  1. kauli kama hizo nyingi za majisifu sana hatuzisikii kwa Simba wala wachezaji wake. Simba wanafanya mambo yao kimyakimya kwa juhudi kubwa wakifuzu husherehekea na wakianguka hawaoni aibu kwasababu hujiwekea akiba kwa kutokujisifu au kubeza wengineo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani nani anajisifu? ameongea kama mchezaji mwenye malengo hakuna mchezaji anayesema watashindwa....kwa hiyo sioni kosa lolote kwa alichokiangalia wewe unaleta ushabiki wako wa makolo kolo

      Delete
    2. Ni kwa kuwa tu kila kukicha ni lazima uwe na kiherehere cha kutaka kujua Jangwani kuna nini, kwani kauli za akina Banda, Kapombe, Boko, Bwalya tunazisikia sana. Na kauli nyingine zimenukuliwa hata katika magazeti ya leo. Huko kukaa kimya unakokusema ni uongo mtupu.

      Delete
    3. Haji kawaingiza Chaka nyie, makolokolo ni yale yaliyopo kwenye jezi ya Utopolo hivyo nyie ndo makolo Ila hamjijui

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic