February 28, 2021


KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos amesema kuwa anasikitika kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Jana, Februari 27 wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold FC ya Mbeya, Carlinhos alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 80.

Aliingia uwanjani dakika ya 66 na alikutana na adhabu hiyo baada ya kumpiga ngumi ya chemba beki wa Ken Gold, Boniface Mwanjonde.

Nyota huyo raia wa Angola amesema kuwa anasikitika kwa alichokifanya kwa kuwa hakutarajia jambo ambalo linampa presha.

"Ninasikitika kwa kadi nyekundu ambayo nimepata hivyo sina la kusema zaidi ya kuomba msamaha kwa kile ambacho kimetokea,".

Kwa upande wake beki Mwanjonde amesema kuwa alikutana na ngumi hiyo ya mbavu baada ya kumziba njia raia huyo wa Angola.

"Ilikuwa ni ngumi ya mbavu baada ya kumzidi spidi yeye alikuja mwilini hapo niliweza kumziba njia na mpira ulitoka nje.

"Wakati tunarudi uwanjani akaja akanipiga ngumi ya mbavu ila niliskia maumivu sio kivile kwa kuwa niliweza kurejea na kuendelea na mchezo,".

Kwenye mchezo huo ambao umeipa Yanga tiketi ya kusonga hatua ya 16 bora bao lilifungwa na Fiston Razack dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti.

8 COMMENTS:

  1. Tushazoea Utopolo ndo mpira wao na asili yao

    ReplyDelete
  2. Ni ngumi ya mkunduni, sasa subiri nýie nguruwe fc mnapigwa za meno

    ReplyDelete
  3. Ni ngumi ya mkunduni, sasa subiri nýie nguruwe fc mnapigwa za meno

    ReplyDelete
  4. Wewe ni mjinga kama huyo mchezaji wako bondia. Sasa matusi ya nini, au unahalalisha watu kupigana ngumi uwanjani? Mtu mwenyewe hana nguvu, hivi tuseme jamaa aliyepigwa angeamua kurudisha ngumi hicho kijamaa chenu kingesalimika na utapiampo wote ule?

    ReplyDelete
  5. Ngumi yenyewe ni sawa na msenge kumpiga mwizi na mto wa sufi akitaraji amemuumiza.

    ReplyDelete
  6. HUYU MCHEZAJI NAYE ANASEMA NGUMI YA MBAVU WAKAWTI WOTE TUMEONA HAIKUA MBAVUNI NAYE AADHIBIWE KWA UONGO ..........tukio la kushangaza kdg kwa sababu wala hakikua na sababu ya Carlos kupaniki ilikua obstruction ya kawaida sana na hata ngumi aliyopiga ni mganga wa kienyeji tu anaweza kusema kwa nini alipiga maana haikua na nguvu sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic