Mwenyekiti wa
Kamati ya kusimamia jengo la klabu ya Yanga Ridhiwani Kikwete, leo ametaja
kamati yake yenye watu nane itakayofanya kazi hiyo
Akizungumza katika
mkutano maalum leo mchana katika Makao Makuu ya Klabu hiyo, Ridhiwani amewataja
wajumbe hao ambapo Makamu wake atakuwa Issa Haji Usi kutoka Zanzibar huku pia
akimjumisha Jaji Mkwawa kuwa mjumbe ambaye aliwahi kuwa naye katika kamati ya
uchaguzi ya klabu hiyo.
Mbali na Mkwawa,
wajumbe wengine ni Baraka Igangula ambaye ni mtaalam wa ramani za majengo, Allan
Magoma, Mavale Msebo, Isaack Chanji na Charles Palapala huku wengine Beda
Tindwa na Mahamoud Milandu ambao watakuwa nje ya kamati hiyo kuu wakiwa na kazi
maalum ya kusaidia mawasiliano ya karibu na wadau watakaohitajika na kamati
hiyo.
Ridhiwani amesema,
lengo la kuchagua kamati hiyo iliyojaa wataalam mbalimbali wa mambo ya benki na
ujenzi, ni kutaka kufanikisha majukumu hayo waliyopewa na Uongozi wa Yanga wa
kulisimamia jengo hilo lililopo mtaa wa Mafia.
“Hii ni hatua ya
awali kabisa, kwa kuanzia leo nimewataja hawa wenzangu ambao tutashirikiana kwa
pamoja katika jukumu hili,kama kamati tutakuwa tunakutana mara kwa mara lakini
sasa tunafikiria kuandaa vikao kama viwili mapema wiki ijayo ili tuweze
kujipangia majukumu ya nani afanye nini,” alisema Ridhiwani








0 COMMENTS:
Post a Comment