Kikosi kamili ya
timu ya Yanga, kimeondoka leo mchana kuelekea Mkoani Tanga, tayari kuwafuata
wenyeji wao JKT Mgambo.
Kikosi kamili cha
Yanga kilichoondoka leo kikiongozwa na Kocha wao Mkuu Ernie Brandts kimewaacha
nyota watano akiwemo Didier Kavumbagu aliyekumbwa na maumivu ya msuli wa
kisigino huku wengine walioachwa na mabeki Juma Abdul,Stephano Mwasyika ambao
nao bado wagonjwa.
Wengine walisalia
jijini Dar ni Omega Seme na makinda watatu walipandishwa kutoka kikosi B Rehani
Kibingu,George Banda na kipa Yusuph Abdul.
Kikosi kamili
kilichowafuata Mgambo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa keshokutwa katika
Uwanja wa Mkwakwani ni pamoja na makipa Ally Mustapha ‘Barthez,’ Said Mohamed
wakati mabeki wakiwa Nadir Haroub ‘Cannavaro,’ Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Oscar
Joshua, David Luhende, Godfrey Taita, Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ na Salum
Telela.
Viungo ni Athuman
Idd ‘Chuji,’Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Frank Domayo, Hamis Kiiza, Nizar
Khalfan, Simon Msuva huku washambuliaji wakiwa ni Said Bahanuzi na Jerry
Tegete.







0 COMMENTS:
Post a Comment