April 19, 2013




Ule upasuaji wa mara ya pili uliokuwa afanyiwe beki wa kati ya Yanga, Mbogo Ladslaus umesitishwa kwa muda.

Kwa mujibu wa Mbogo, angalau miezi miwili itapita bila ya kufanyiwa upasuaji huo na madaktari watafanya kazi ya kuchunguza.


Akizungumza na Salehjembe leo jijini Dar, Mbogo alisema daktari wa Yanga, Nassor Matuzya amemueleza kwamba wanahitaji muda.

“Dokta amesema wataangalia kwanza, kwamba kama kila kitu kinakwenda kama walivyotaka hata upasuaji wenyewe unaweza usifanyike.

“Inaweza ikachukua miezi miwili au zaidi ili kupata jibu la uhakika kuhusiana na nini kinatakiwa kufanyika,” alisema Mbogo.

Mbogo alifanyiwa upasuaji wa kwanza kuondoa uvimbe kwenye paji lake na ulikuwa wenye mafanikio makubwa.

Lakini baadaye ilielezwa kwamba lazima ufanyike upasuaji wa pili ili kuweka mambo vizuri.

Beki huyo alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Toto African ya Mwanza ambayo sasa inahaha kubaki Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic