April 21, 2013



Kiungo wa Mkenya, Victor Wanyama ameingia katika rekodi ya kuwa mmoja wa wachezaji waliobeba ubingwa msimu huu.


Wanyama na Celtic wamebeba ubingwa wa Ligi Kuu Scotland (SPL) baada ya kuichapa Inverness kwa mabao 4-1 katika mechi yao ya leo.


Wanyama ambaye amekuwa tegemeo katika kiungo cha timu hiyo alikuwa kati ya wachezaji waliocheza vizuri.

 Hooper alifunga mabao mawili katika dakika ya 61 & 73, mengine mawili yakafungwa na Ledley dakika ya 66 na Samaras, 88.

Wanyama amekuwa gumzo kati ya viungo wanaowania na klabu kubwa mbalimbali kama Manchester United na Arsenal ingawa inaonekana ataendelea kubaki Uskochi.

1 COMMENTS:

  1. mkuu mbona sielewi wanyamba.wanyama niaje jooo au ni watu wawili ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic