Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil itakuwa
michuano ya kwanza ya soka kuonyeshwa katika mfumo wa Ultra HD.
Teknolojia hiyo tayari imeanza kutumika ingawa
imeonekana kuwa ya wachache kutokana na televisheni zenye mfumo huo kuuzwa kwa
bei ghali zaidi.
Mfano televisheni ya LG ya Ultra HD ya Inchi 84
inauzwa hadi pauni 20,000 (zaidi ya Sh milioni 52).
Lakini makampuni yanayotengeneza yameeleza kuanza
katikati ya mwaka juu zitaanza kupatikana madukani hadi kuanzia pauni 5,000.
Lakini michuano hiyo ya Kombe la Dunia ndiyo
itatumika kuitangaza zaidi teknolojia hiyo ambayo inaelezwa ubora wa picha zake
ni mara nne kuliko unaoonekana katika televisheni za sasa.
Kwa upande wa Afrika inaonekana televisheni hizo
huenda zikapata soko la chini kutokana na ukubwa wa bei kwa kuwa watakaonunua
ni wachache walizonazo.
Hata hivyo, Waafrika wengi watakuwa na hamu ya
kuzitumia huku waiweka matarajio yao makubwa kwa Mchina ambaye anaweza ‘kuchakachua’
na mambo yakaenda kama Ulaya tu.









0 COMMENTS:
Post a Comment