Mechi kati ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga na wenyeji wao
Polisi Moro imeingiza Sh milioni 36.6.
Polisi Moro na Yanga, zilitoka sare ‘tasa’ katika mechi
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, juzi Jumamosi.
Watazamaji 7328 waliingia katika mechi hiyo na kulipa viingilio
vya Sh 5,000.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Morogoro (MRFA), Hamis Semka amesema
Sh 36, 640,000 zimepatikana katika
mchezo huo na tayari mgawo umefanyika.
Alisema mgawo umefanyika katika makundi saba ambayo ni wenyeji Polisi Moro SC na wageni wao Yanga, kila
upande ulipata Sh 8,207,472, Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) ikapewa Sh 5,589,152.
Mfuko wa Maendeleo ya mpira wa miguu (FDF) ukalamba Sh 2,503,976.17.
Gharama za uwanja ni Sh 4,173,293, gharama ya tiketi ni Sh 2,548,890 na Sh Sh 2,503,976 zikaenda kwenye kamati ya ligi.
Gharama za uwanja ni Sh 4,173,293, gharama ya tiketi ni Sh 2,548,890 na Sh Sh 2,503,976 zikaenda kwenye kamati ya ligi.
Katika mechi hiyo, Yanga walicheza vizuri katika kipindi cha
pili kabla ya Polisi kubadilika katika kipindi cha pili na kuwa mwiba mkali.
0 COMMENTS:
Post a Comment