Arsenal
imejadili suala la kutaka kumchukua mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney
ambaye anaonekana kutokuwa na furaha.
Hata
kabla ya mwaka mmoja baada ya kumuuza Robin van Persie kwa Manchester United,
Arsenal imeona inaweza kumnasa Rooney ili kuongeza nguvu katika safu yake ya
ushambuliaji.
Baada
ya kikao hicho, inaonekana siku chache zijazo, Arsenal watakutana na wahusika wa
United na kujadili suala la Rooney ambaye aliomba kuuzwa.
Lakini
swali au mjadala mkubwa ni kiasi cha mshahara anacholipwa Rooney kwa wiki
ambacho ni pauni 250,000 kama kweli Arsenal wataweza kukilipa.
Mfano
mchezaji kama Lukas Podolski analipwa pauni 100,000 kwa wiki, hivyo huenda
kukawa na ugumu kwa klabu hiyo ya London.
Kingine
ni swali, kama kweli Rooney atakubali kwenda Arsenal ambayo imekuwa inaonyesha
haina njaa ya vikombe.
0 COMMENTS:
Post a Comment