Liewig akiwa na Julio |
Amesema anatarajia kurejea nchini mwezi ujao ili kuanza maandalizi ya kuinoa timu hiyo.
Akizungumza moja kwa moja kutoka Ufaransa, Liewig amesema bado ana mkataba Simba na hajui lolote kuhusu kuachishwa kazi.
“Sijui
lolote, nimeona kwenye vyombo vya habari kupitia mtandao, lakini sioni kama
kuna sababu ya kuuliza.
“Taratibu
za kazi zinajulikana, mimi ni mwajiriwa na sipaswi kuhoji mambo mengi. Kama huo
utakuwa uamuzi wao, basi kuna taratibu za kufuata,” alisema akiwa nchini
Ufaransa.
Liewigi
amesema yuko mapumzikoni, hivyo atawasiliana na uongozi wa Simba baada ya siku
chache ili kupata uhakika.
Tayari Simba
imefikia makubaliano na Abdallah Kibadeni ambaye alikuwa Kocha wa Kagera Sugar.
Liewig
alichukua nafasi ya Milovan Cirkovic lakini ameonekana kufeli zaidi baada ya
timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika ligi kuu.
Hata hivyo,
uongozi wa Simba kupitia Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’,
imesema haimhitaji tena Mfaransa huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment