Baada ya kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kukabidhiwa vazi la suti na wadhamini kinywaji cha bia ya Kilimanjaro, limeonekana kama jambo jipya.
Lakini hii
si mara ya kwanza kwa Stars kukabidhiwa suti, ingawa ninaweza kusema
zilizotolewa safari hii ziko katika kiwango kinachovutia zaidi.
Stars
walikabidhiwa suti na Serengeti waliokuwa wadhamini wakati huo na wachezaji
walitilia viwalo na kupendeza kwelikweli.
Ulionekana
ni mfano mzuri na kwamba walikuwa wanakwenda kimataifa zaidi na mambo
yangebadilika zaidi.
Lakini baada ya kurejea kutoka Chan, sikuwahi tena kuiona Stars ikisafiri ikiwa imevaa suti hizo.
Badala
yake walirudi katika mtindo wa ‘trak suti’, nikajua ilikuwa ni kubadilisha
mazingira, hadi leo kimya.
Nimeandika
makala haya, lengo likiwa ni kuwakumbusha TFF ambao ndiyo walezi na
wanaohangaika na timu hiyo vizuri zaidi kwamba wanapaswa kupambana na
kuhakikisha suti hizo zinaendelea kuwepo.
Ni vazi la
heshima la kikosi, hivyo wanapaswa kuwa nalo kwa kipindi kirefu kwa kuwa bado
timu yetu inasafiri.
Wadhamini wameonyesha
wanajali, walichofanya ni kitu kikubwa, hivyo kama nazo zitayeyuka baada ya
muda mfypi halitakuwa jambo zuri.
Jezi mnaweza
kubadilishana, kwa kuwa ndiyo mfumo wa kisasa katika soka. Lakini haiwezekani
kubadilishana suti hizo.
Ndiyo maana
nasisitiza vema zikatunzwa ili kuendelea kuifanya Stars ikiwa katika mfumo
tofauti na kuongeza mvuto kwa wadau wa soka nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment