Siku kama
ya leo, Mei 17 inakumbukwa kama moja ya siku ya majonzi katika historia ya
klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Simba
wanaotumia rangi nyekundu na nyeupe, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi walimpoteza
kiungo wao, Patrick Mutesa Mafisango raia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) katika ajali mbaya ya gari.
Gari lililosababisha kifo chake.. |
Gari hilo
liligonga mti katika eneo la Veta Chang’ombe, mwendo wa dakika tatu kutoka
nyumbani kwake Keko jijini Dar.
Alipata
ajali hiyo wakati akitoka katika misele ya usiku na wenzake, inaelezwa alikuwa ‘maji’
wakati gari aina ya Toyota Cresta Mark II lilipomshinda na kugonga miti miwili.
Boban akiingia mochwari na Kokoo, nyuma kaka yake Idd Moshi Myamwezi |
Mafisango
aliumia vibaya na kukimbizwa Muhimbili lakini ilikuwa vigumu kuokoa maisha
yake.
Ilikuwa usiku
wa kuamkia Alhamisi Mei 17, 2012. Ndiyo leo, Mei 17,2013, Simba imetimiza mwaka
sasa bila ya kiungo huyo.
Niyonzima akiwa haamini baada ya kuuona mwili wa marehemu mochwari, kulia ni Uhuru Selemani aliyekuwa akilia kwa sauti ya juu |
Simba
itacheza mechi ya pili dhidi ya watani wake bila ya kuwa na Mafinsango, mechi
ya kwanza ikiwa ni ile ya Oktoba 3, 2013 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1. Mechi
ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa ni ile ambayo Wekundu wa Msimbazi
walishinda kwa mabao 5-0.
Mashabiki wa
Simba wanaendelea kumkumbuka Mafisango kutokana na umahiri wake wakati akiwa
mchezaji wa Simba na msaada mkubwa aliokuwa akiutoa.
Ilielezwa Mafisango
ndiye alitoa mchango mkubwa kwa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ kubadilika na
kujali zaidi kazi yake.
Wakati akiwa
Simba, Mafisango alikuwa rafiki wa karibu wa Boban na kwa kiasi kikubwa
alimbadilisha na kumfanya arudi na kucheza soka.
Uthibitisho,
hata wakati wa msiba, Boban ndiye alionekana kuguswa zaidi, alilia kutaka
kuingia mochwari ili kuhakikisha kama kweli swahiba wake alifariki dunia.
Lakini aliomba
ruhusa na kuondoka katika kikosi cha Taifa Stars, alisafiri hadi Kinshasa, DR
Congo kwenda kumzika Mafisango.
Mafisango atakumbukwa
kwa mengi ikiwamo utukutu wake, lakini uwezo mkubwa wa kusakata soka ndiyo
unabaki kwua gumzo hadi leo.
RIP.
0 COMMENTS:
Post a Comment