Pamoja
na kufanya ni siri kubwa, taarifa
zinaeleza Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuondoka Pemba leo
jioni.
Imeelezwa
Yanga watatua moja kwa moja mjini Bagamoyo tayari kujiandaa kuja Dar es Salaam
kesho.
Wakiwa
mjini Bagamoyo, Yanga watafikia katika hoteli ya kitalii na watapumzika hadi
kesho watakapoanza safari ya kuja Dar es Salaam.
Mwandishi
wetu wa Pemba amethibitisha hilo kwamba Yanga watatulia Bagamoyo kwa siku moja
kabla ya kuanza safari ya kurudi Dar kesho tayari kwa mechi.
Kwa
upande wa Simba, kikosi chao kinatarajia kutua na ndege leo jioni kikitokea
Zanzibar.
Simba
watalala Dar es Salaam, tayari kwa mechi hiyo ya kesho ambayo tayari ni gumzo
kila sehemu.
0 COMMENTS:
Post a Comment