Kumekucha,
inaonekana kuna vita kali kati ya Yanga na timu ya Tunisia kuhusiana na
kumsainisha Haruna Niyonzima.
Kiungo
huyo amekuwa akiusumbua uongozi wa Yanga kwa takribani wiki moja sasa wakitaka
asaini, naye anapiga chenga.
Awali
kulikuwa na taarifa kwamba Niyonzoma alitaka kusaini Simba, lakini baadaye
kumekuwa na taarifa ameamua kuachana na Msimbazi.
Ushindani
umebaki kati ya Yanga na timu ya Tunisia ambayo amekataa kuitaja,.
“Kweli
kuna timu ya Tunisia inanitaka, imenipa ofa nzuri lakini ninachotakiwa ni
kutulia kwanza.
“Kwa sasa
bado ni mchezaji wa Yanga, hivyo ninapaswa kutulia kama binadamu na kujua nini
nitakifanya,” alisema Niyonzima.
Lakini
taarifa nyingine za jana, zilieleza mmoja wa ‘majembe’ ya usajili ya Yanga,
Abdallah Bin Kleb alikuwa anafanya juhudi za kuhakikisha anampata Niyonzima
asaini Yanga kabla ya kuondoka.
Kiungo huyo
raia wa Rwanda amekuwa gumzo kwa misimu miwili sasa tokea atue Yanga akitokea
APR ya kwao Rwanda.
Hali hiyo
inatokana na kuonyesha uwezo mkubwa na kuwa msaada mkubwa katika kiungo cha
Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment