Kocha Mkuu wa Manchester City, Roberto Mancini ameingia
hofu ya kazi yake baada ya uongozi wa klabu hiyo kukutana na wakala wa kocha wa
Malaga, Manuel Pellegrini.
Pellegrini amekuwa kati ya makocha waliokuwa
wanatakiwa na Man City kwa kipindi kirefu sasa, lakini safari hii inaonekana
wamepania kumchukua.
Mkurugenzi wa soka wa Man City, Txiki Begiristain alikutana
na wakala huyo katika chakula maalum cha mchana jijini Madrid, siku chache
zilizopita.
Pamoja na kuwa Mancini alihakikishiwa nafasi hiyo
msimu ujao na Mwenyekiti wa Man City, Khaldoon Al Mubarak, bado ameonekana kuwa
na hofu kutokana na mkutano huo wa Madrid.
“Kiasi
fulani inachanganya, ila siwezi kuwa na hofu kwa kuwa ndani ya msimu miwili
tumepata vikombe vitatu. Mara moja mabingwa FA na ubingwa ligi kuu.
“Lakini angalia leo tuko katika nafasi ya pili na
nachanganyikiwa kwa kuwa nilitaka kushinda ubingwa mwingine wa England. Lakini sijui,
nafikiri swali hilo unaweza kumuuliza Txiki akafafanua vizuri,” alisema
Mancini.
Hali hiyo inazidi kumpa hofu Mancini, lakini bado
inaonyesha kocha huyo wa Mallaga anapewa nafasi ya kurejea Madrid kama Jose
Mourinho ataondoka na kurejea Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment