May 1, 2013



Mashabiki wa timu inayoshiriki Ligi ya Mkoa wametoa kali nchini Serbia baada ya kuchimba kaburi katikati ya uwanja wa soka na kuandika, “daraja la pili au hiki”.

Maandishi hayo yaliandikwa katika jiwe maalum ambalo huwekwa katika kaburi mara baada ya mazishi kufanyika.

Hali hiyo ya mashabiki kutoka Serbia ambaye ni nchi anayotokea kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic imeonyesha kuwashangaza wengi wakiwemo waliosoma kuhusiana na stori hiyo nchini England.

 

Mashabiki hao wa timu ya Macva Sabac wameonyeshwa kuchoshwa na timu yao kushindwa mara kadhaa kusonga hadi daraja la pili.
Milovan anatokea katika eneo la Cacak ambalo linatamkwa “Chachak”, wakati timu ya Macva Sabac inatokea katika eneo la Sabac na imeshindwa kupata nafasi hiyo kwa miaka sita mfululizo ikipungukiwa pointi chache tu.
Mashabiki hao wanasisitiza kwamba wanata kuiona ikifuzu kwa kuwa imebakiza mechi nne za kucheza, lakini ina pointi nne tu nyuma ya viongozi wa ligi.
Hofu ya mashabiki ni kwamba, timu yao imekuwa ikivuruga katika hatua za mwisho kabisa kwa miaka sita mfululizo ndiyo maana wameamua kutoa onyo kwa kuchimba kaburi hilo katikati ya uwanja wao.
Mmoja wa maofisa wa timu hiyo, Zvone Jovanovic ameshangazwa na kusema: “Kwa miaka minne ilibaki kidogo tupande daraja la pili, tukakosa pointi chache sana. Lakini sijui kwa nini wamefikiria kitu cha namna hii.
“Nafikiri timu inastahili utulivu badala ya vitisho kwa kuwa tuna pointi nne tu nyuma ya vinara wa ligi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic