Luis
Suarez ameonywa na mkewe na kutakiwa kubadilika mara moja kwa kuachana na tabia
aliyoifanya.
Mkewe
Suarez aitwaye Sofia amemtaka mumewe kubadili tabia ili kurudisha heshima yake
kwa jamii inayoonekana kupotea.
Suarez
,26, amesimamishwa mechi kumi kutokana na kumuuma beki Branislav Ivanovic wa
Chelsea.
Pamoja
na kumuomba abadilike, mkewe amemsisitiza lazima ajifunze kujizuia kutokana na
suala la hasira hasa zile za papo kwa hapo ambazo zimekuwa zikimuathiri.
Katika mahojiano na jarida la Liverpool, Suarez alisema: “Mke
wangu ameniambia kuwa ninabishana sana na waamuzi na mabeki na inawezekana
ndiyo maana ninakuwa na hasira kupita kiasi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment