Kocha
Mkuu wa Barcelona, Tito Vilanova amesema mshambuliaji wake, Lionel Messi hakuwa
mgonjwa.
Vilanova
amesema alilazimika kumuacha nje Messi baada ya kusema alikuwa anajisikia
vibaya, hivyo akaamini asingeweza kuisaidia timu.
Barcelona
ilikumbana na kipigo cha aibu cha mabao 3-0 katika mechi ya pili ya nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo kufanya iwe imeondolewa na Bayern
Munich kwa jumla ya mabao 7-0 ambayo ni rekodi mpya.
Messi
alionekana katika benchi wakati Barcelona ikipambana na Wajerumani hao ambao
ndiyo walitawala mchezo utafikiri wako nyumbani.
Wengi
walitarajia kumuona Messi akiingia ili kuokoa jahazi, lakini badala yake,
Vilanova alianza kuwatoa wachezaji tegemeo kama Xavi na baadaye Iniesta ikiwa
ni dalili ya kukubali hawana ujanja dhidi ya Bayern maarufu kama Bavarians.
“Jana (juzi) alifanya mazoezi na timu na ilionekana angecheza lakini baadaye mambo yakabadilika pia, ndiyo maana nasema hakuwa majeruhi, lakini niliona kutokana na hali hiyo asingekuwa msaada kwa timu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment