Wachezaji 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen
kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini
ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).
Kocha Kim amewaitaka wachezaji katika kambi hiyo ya
siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata
baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.
Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya
timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula,
David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na
timu yao ya Azam.
0 COMMENTS:
Post a Comment