Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam
kupokea na kupanga utekelezaji wa maagizo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)
kuhusu uchaguzi wa shirikisho.
Kikao hicho cha dharura chini ya
Uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika
kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo ya Fifa unafanyika haraka ili uchaguzi
ufanyike ndani ya muda uliopangwa.
Fifa katika maelekezo yake imetaka
kwanza ziundwe Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili kabla ya
kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF.
Fifa imeagiza uchaguzi uwe umefanyika kabla ya
Oktoba 30 mwaka huu.
Tayari shirikisho hilo lililotuma
wajumbe wake hivi karibuni kuja nchini kutatua mgogoro wa uchaguzi wa TFF na
tayari limeagiza kurudiwa kwa mchakato huo.
TFF kukutana, maana yake watajadili
ambayo walielezwa na kutakiwa kuyatimiza ili kufanya mambo yaende katika
mstari.
Wagombea wote wakiwemo wale
waliokuwa wameondolewa wamekubaliwa kuchukua fomu na kugombea.
0 COMMENTS:
Post a Comment