Mechi namba 172 ya Ligi Kuu ya
Vodacom kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa juzi (Mei 1 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare
ya bao 1-1 imeingiza sh. 66,022,000.
Watazamaji 11,478 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,378,927.45 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,071,152.54.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho
kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 10,230 na
kuingiza sh. 51,150,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio
cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 69 na kuingiza sh. 1,380,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 7,819,793.62, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi
sh. 4,691,876.17, Kamati ya Ligi sh. 4,691,876.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 2,345,938.09 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 1,824,618.51.
SOURCE: TFF
0 COMMENTS:
Post a Comment