Kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata Real Madrid kutoka kwa wapinzani wao
wakubwa Atletico Madrid kimemfanya kocha Jose Mourinho kumaliza msimu bila hata
kombe moja.
Mechi hiyo ya fainali ya Copa del Rey ilimalizika kwa Atletico kushinda
kwa mabao 2-1 ikitokea nyuma baada ya Madrid kupata bao katika dakika ya 14.
Diego Costa ndiye alisawazisha kwa Atletico kabla ya beki Mbrazil,
Miranda kufunga bao la pili katika 99 baada ya mechi kwenda katika dakika 30 za
nyongeza.
Mechi hiyo ilijaa vituko huku mara kwa mara Real Madrid wakilalamika
kuhusiana na uamuzi wa refa ambaye alionekana mara kadhaa kuacha faulo
zilizotakiwa kuelekezwa Atletico Madrid.
Mwamuzi huyo alimtoa nje Mourinho kwa madai ya kuonyesha utovu wa nidhamu
lakini akamtoa Ronaldo kwa kumchezea rafu makusudi mchezaji wa Atletico ingawa
picha za video zilionyesha Ronaldo alianza kufanyiwa madhambi kwa kuchotwa
mtama lakini mwamuzi akauchuna.
Hata hivyo, bado Madrid wanapaswa kujilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi
zikiwemo zile kupitia Ronaldo, Benzema na Ozil ambazo zingeweza kuwapatia
mabao.
Madrid imemaliza msimu bila kuwa na kombe na Mourinho tayari
amethibitisha kuondoka, taarifa zinaeleza anarejea Chelsea ya England ambayo
mkononi ina kombe la Europa League.
0 COMMENTS:
Post a Comment