Holiday Inn |
Protea Oysterbay.. |
Kila kitu kimekuwa ni siri, kambi za Simba na Yanga sasa zimehamia
jijini Dar es Salaam.
KAMBI YA SIMBA:
Awali Yanga walitaka kwenda Bagamoyo, lakini imeonekana kesho watakuwa
na safari kurejea jijini Dar es Salaam.
KAMBI YA YANGA:
Sasa Yanga waliokuwa wameweka kambi mjini Pemba wako Dar es Salaam
katika hoteli tulivu ya Protea Osyterbay ambako wachezaji wamepumzika kusubiri
mechi ya kesho dhidi ya Simba.
Lakini Simba nao, wamerudi Dar pia wakitokea Unguja na kuweka kambi
katikati ya jiji katika hoteli ya Holiday Inn ambayo miaka miwili iliyopita,
Yanga waliweka kambi hapo.
Hoteli hizo za kitalii ni nadra kwa Yanga au Simba kukaa, lakini safari
hii inaonyesha kiasi gani kila upande umepania kushinda mechi hiyo, hivyo suala
la gharama si ishu kubwa tena kwao.
Umbali kutoka Oysterbay iliko Protea na Upanga, katikati ya jiji ilipo
Holiday Inn si mkubwa. Takribani mwendo wa dakika sita au saba kwa gari
linalotembea taratibu.
Usiri umeendelea kuwa mkubwa sana kila timu ikionyesha haitaki kuonyesha
iko wapi ingawa ni sehemu za kisasa ambazo wangependa wajulinake wako hapo.
Imekuwa kawaida inapokaribia mechi ya watani, mara nyingi hisia za
hujuma hutangulia hata zinapokuwa hazipo, ili mradi uoga na tahadhari kubwa
inachukua nafasi.
Inawezekana kabisa kutokana na maeneo zilipoweka kambi, timu hizo kesho
zikapita njia moja kwenda Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kipute chao.
0 COMMENTS:
Post a Comment