Kiungo
mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa ameahidi kufunga bao moja katika mechi ya
kesho dhidi ya Yanga.
Simba
na Yanga zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar katika mechi inayotarajiwa
kuwa ya kusisimua.
Lakini
gumzo ni Ngassa ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga ambayo
atakutana nayo hiyo kesho.
Msemaji
wa Simba, Ezekiel Kamwaga amewaambia waandishi wa habari leo kwamba, taarifa za
Ngassa kasaini Yanga au la, hawezi kuzikanusha au kuthibitisha lakini mchezaji
huyo ameahidi kufunga bao hiyo kesho.
“Ngassa
ni kati ya wachezaji waliofanya vizuri katika mazoezi yetu kule Zanzibar, kwa
kifupi taarifa hizo za Yanga wala hazijamchanganya ingawa siwezi kusema ndiyo
au la kuwa amesaini.
“Lakini yeye ameahidi kuwa atafunga bao moja
kesho, ila suala la kumpanga au kutokumpanga linabaki kwa kocha Liewig,”
alisema Kamwaga.
Gazeti
maarufu la Michezo la Championi ndilo liliandika stori ya Ngassa kusaini Yanga
kwa miaka miwili.
Maana
yake, baada ya mechi ya keshokutwa, moja kwa moja atajiunga na timu yake mpya.
Tayari
mmoja wa viongozi wa Yanga amethibitisha Ngassa kujiunga na Yanga na
anatarajiwa kutambulishwa mara moja baada ya mechi hiyo ya kesho.
0 COMMENTS:
Post a Comment