Mafisango wa pili kulia waliosimama akiwa na kikosi cha Simba msimu uliopita.. |
Wachezaji na waamuzi katika mechi ya kesho kati ya Yanga na Simba, watasimama dakika moja kutoa heshima na kumkumbuka aliyekuwa kiungo wa Simba, Patrick Mutesa Mafisango.
Mafisango
raia wa DR Congo alifariki dunia Mei 17, 2012 katika ajali ya gari iliyotokea
eneo la Veta Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Msemaji
wa Simba, Ezekiel Kamwaga amewaambia waandishi wa habari leo kuhusiana na
dakika moja hiyo kwa lengo la kumkumbuka na kumpa heshima Mafisango.
Wachezaji
wa Simba watavaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka
kiungo huyo.
Wakati
wa uhai wake, Mafisango ambaye aliichezea Azam FC pia, alikuwa kiungo tegemeo wa
Simba ambaye alileta mabadiliko makubwa kiuchezaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment