Mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba
itaonyeshwa moja kwa moja na Chaneli ya Super Sport 9.
Ofisa Mauzo
wa DStv Tanzania, Furaha Samalu amesema mechi hiyo ya kesho kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam itaonekana katika nchi zaidi ya 30 barani Afrika.
“Kweli
tutaonyesha mechi hiyo, kila kitu kimekwenda vizuri na tunachosubiri ni mchezo
tu,” alisema Furaha.
Mechi kati
ya Yanga na Simba ni moja ya zile zilizo kubwa zaidi barani Afrika.
Mashabiki wengi
Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wamekuwa na hamu ya kuiona mechi hiyo moja
kwa moja.
Tayari joto
lake liko juu na mashabiki wamekuwa wakihaha jijini Dar es Salaam kutafuta
tiketi kwa ajili ya mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment