Kocha wa Man United, David Moyes anaanza kazi rasmi keshokutwa Jumatatu lakini presha kubwa ni mshambuliaji wa timu hiyo, Wayne Rooney.
Kocha huyo wa zamani wa Everton ana mpango wa kuzungumza naye na kumshawishi aendelee kubaki Old Trafford.
Moyes anataka kumueleza Rooney asahau tofauti zao na kocha wa zamani Alex Ferguson ili aendelee kufanya kazi na kikosi chake. Hofu imekuwa ni muonekano wa Rooney katika sehemu mbalimbali.
Taarifa zinaeleza Moyes amekuwa na hofu kwamba Rooney anaonekana ana nia ya kweli kuondoka United na huenda akampa Moyes jibu la kwamba anasisitiza anataka kuondoka.
Rooney, 27, amekuwa akiwaniwa kwa ukaribu zaidi na Kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho pia Arsene Wenger wa Arsenal.
Lakini mwenyewe ameishaeleza kwamba ana nia siku moja acheze katika kikosi cha Barcelona.
Hali hiyo inampa presha Moyes kwa kuwa inaonekana kama kumbakisha kwake itakuwa ni mafanikio makubwa kwake ya kukituliza kikosi chake na kuanza ushindani mkali wa kuvaa viatu vya Ferguson.
0 COMMENTS:
Post a Comment