Arsenal iko katika hatua za mwisho kumsajili kipa namba moja wa Brazil, Julio Cecar.
Cecar anakipiga katika kikosi cha Queens Park Rangers ambacho tayari kimeporomoka hadi Ligi Daraja la Kwanza England.
Kipa huyo ameendelea kuomyesha uwezo mkubwa na kuisaidia Brazil kuvuka hadi hatua ya Kombe la Mabara.
Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger anamtaka kipa huyo ili kuongeza ushindani dhidi ya makipa wengine alionao ambao ni Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Tayari Arsenal imeshawaeleza QPR nia yao ya kumnasa kipa huyo lakini kila kitu kimesimamishwa kwa kuwa Cesar anaitumikia Brazil na ataiongoza katika mechi ya fainali dhidi ya Mabingwa wa Dunia Hispania, kesho.
Awali Wenger alitaka kumsajili kipa wa Stoke Asmir Begovic ambaye ameshapata ulaji mwingine au yule wa Liverpool, Pepe Reina lakini sasa anaonekana kubadili welekeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment